WANAJESHI NCHINI IVORY COAST WAANDAMANA HUKU WAKIFYATUA RISASI | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Friday, 12 May 2017

WANAJESHI NCHINI IVORY COAST WAANDAMANA HUKU WAKIFYATUA RISASI





Wanajeshi walioasi nchini Ivory Coast walizingira makao makuu ya jeshi jijini Abidjan siku ya Ijumaa na kufwatua risasi hewani baada ya msemaji wa jeshi kuomba radhi kwa maandamano yaliyotokea mapema mwaka huu.
























Hatua hii imekuja baada ya wanajeshi hao usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa kufwatua  risasi hewani katika kambi yao mjini Bouake ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo.
Siku ya Alhamisi, Fofana, msemaji wa wanajeshi  8,400 waliomsaidia rais Alassane Ouattara kuingia madarakani mwaka 2010, alijtokeza na kusema kuwa wanajeshi hao wanaomba radhi na wameachana na mpango wao wa kuendelea kushinikiza kulipwa fedha zao.


Waasi hao wa zamani ambao sasa ni wanajeshi wamekuwa wakidai kulipwa Euro 18,000 kwa kile mwanajeshi, lakini walifanikiwa kupata Euro 7,500 na ripoti zinasema kuwa ilikuwa imepangwa kuwa watapokea malipo mengine mwezi huu.
Hata hivyo, baadhi ya wanajeshi walijitokeza baadaye na kudai kuwa hawakushauriwa kuhusu hatua iliyofikiwa na msemaji wao.
Rais Outtara amekuwa akisema kuwa nchi yake inapitia kipindi kigumu cha kisiasa kwa sababu ya kushuka kwa biashara ya Cocoa.
Tukio la Ijumaa, limezua hali ya wasiwasi jijini Abidjan huku shughuli zikisitishwa na wafanyibiashara kufunga biashara zao.

google+

linkedin