Ndege ya kibinafsi iliyowabeba watu hao iliwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Ijuma asubuhi.
Maafisa nchini Kenya wanasema walikuwa wanafahamu kuhusu kurejeshwa kwa raia wa nchi hizo mbili, na tayari raia wa Somalia wamerejeshwa mjini Mogadishu kwa kutumia ndege nyingine ya kukodi.
Hatua hii ilitarajiwa kutokana na operesheni inayoendelea nchini Marekani kuwarudisha nyumbani wahamiaji haramu wanaoishi nchini humo lakinia pia wageni wanaojihusisha na makosa mbalimbali.
Mwezi Januari ,wakenya wawili na raia wengine 90 wa Somalia walirejeshwa walifukuzwa Marekani kwa sababu mbalimbali.
Rais Donald Trump miezi kadhaa iliyopita, aliamua kuwazuia wahamiaji kutoka mataifa ya Kiislamu kuingia nchini humo, hatua ambayo ilizuiwa na Mahakama.
Mataifa yaliyolengwa ni pamoja na Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen.