Baraza la usalama la UN kuiongezea vikwazo Korea kaskazini | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Saturday 5 August 2017

Baraza la usalama la UN kuiongezea vikwazo Korea kaskazini

media

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linataraji kupigia kura rasimu ya azimio kuiongezea vikwazo Korea kaskazini,kwa mujibu wa wanadiplomasia.


Pendekezo hilo litapiga marufuku uingizwaji wa bidhaa ambapo Pyongyang itapoteza kiasi cha dola za Marekani bilioni moja katika mapato yake ya mwaka.

Baada ya mwezi wa majadiliano Marekani ilifikia makubaliano na China,ambayo ni mshirika muhimu wa kibiashara wa Korea kaskazini kuhusu mpango wa kushinikiza taifa hilo kusitisha mpango wake wa kufanya majaribio ya makombora.

Zoezi la upigwaji kura linatarajiwa jumamosi jioni kwa mujibu wa wanadiplomasia.

google+

linkedin