BAADHI YA SIRI ZILIZOFANYWA NA CIA (MAREKANI),HUWEZI KUZIJUA | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Saturday 5 August 2017

BAADHI YA SIRI ZILIZOFANYWA NA CIA (MAREKANI),HUWEZI KUZIJUA



1.Kuanzia miaka ya 1950 hadi mwaka 1973 CIA walianzisha mradi ulioitwa MKULTRA ukiwaa na lengo la kuwapandikiza watu vitu kwa ajili ya kuwasimamia kiakili,Ambapo CIA walitumia njia kama madawa,vifaa vya umeme,kuwanyima hisia watu n.k (sensory deprivation) pamoja na kufanya mateso makali kupitia kisaikolojia kwa watu waliokua wanawafanyia majaribio ,na taasisi tofauti zipatazo 80 zilikumbwa na mkasa huu kama vyuo ,hospitali,magereza,na makampuni ya madawa na kuna mtu ambaye alikua mhusika wa haya ambaye alikua Harvard 1950 alijulikana kama Theodore Kaczynsk .Mwaka 1995 raisi Clinton aliomba msamaha kwa niaba ya serikali ya marekani ,msimamizi wa CIA aliharibu faili la mradi huu mwaka 1973 na bado haijafahamika zaidi nini kilitokea katika majaribio haya.raia wa marekani na canada pia waitumia wafungwa waliowakamata kutoka vita na korea.Lengo kuu la huu mradi ni kuwatumia watu bila wao kujua dhidi ya umoja wa kisoviet,china,na korea ya kaskazini pia walihitaji kumdunga madawa haya fidel castro ili awe chini yao.kama uliwai angalia series ya iris au yeyote kuna sindano unachomwa alafu unaanza kuongea vyote sasa ndio njia ambazo CIA walibuni kuwadhibiti wapelelezi au makachero wa kisoviet.
Hiyo hapo iliondikwa LSD ukidungwa utazungumza vyote aisee
HAWA JAMAA NI SHIDA



2.wakuu wa majeshi ya marekani wakati wa utawala wa J.kennedy walipanga  kufanya njama ya kumvamia fidel castro kupitia njia ya kutengeneza picha ya kua castro amefanya ugaidi ndani ya marekani ili wapate kuungwa mkono na raia wa marekani njia walizopanga kutumia ni kama kuwaua wamarekani ndani ya mitaa pia kuhusisha boti iliyobeba wakimbizi ikitoka cuba na kuzamishwa ndani ya maji ya bahari yenye kina kirefu pia kufanya ugaidi ndani ya jiji la washington,kuteka ndege au kitaalamu hijack,Njia mbaya zaidi ambayo mkuu wa kitengo cha jeshi  Lyman Lemnitzer alipanga ni kuhusisha ndege ya jeshi la cuba ikivamia wanafunzi  wa chuo.lakini mwisho wa siku JFK aligoma mpango huu na kitaalamu ilijulikana kama Operation Northwoods ambayo ilikua mwaka 1962 na CIA Ndio waliopendekeza mpango .Mpaka hapa awa watu hawana uruma na raia wao.


 3.Pia CIA walikuja na mpango ulioitwa Operation MockingbirdIn mwishoni mwa miaka ya 1940 wakiwa na lengo la kuvinunua na kuvisimamia vyombo vya habari ,pia walitaka kuwa na wanahabari wao moja kwa moja watakao kua chini yao wabunifu wa huu mpango ni kama wafuatao Frank Wisner, Allen Dulles, Richard Helms, and Philip Graham (publisher of The Washington Post) vyombo hivi ni kama ABC, NBC, CBS, Time, Newsweek, Associated Press, United Press International (UPI), Reuters, Hearst Newspapers, Scripps-Howard, and Copley News Service.hadi kufikia miaka ya 1950 walikua wamefanikiwa na zoezi lao la kusimamia vyombo hivi vya habari wakiwa na lengo la kutoa habari za uongo na propaganda.Nazani umeshuhudia habari hizi toka iraq na syria na libya.

SINA LA ZAIDI,
SHARE KAMA UMEPENDA.
IMELETWA NA  ,
VASILY RICHARD  



google+

linkedin