Watu zaidi ya 7 wajeruhiwa kwa risasi nje ya msikiti Ufaransa | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Monday, 3 July 2017

Watu zaidi ya 7 wajeruhiwa kwa risasi nje ya msikiti Ufaransa

media

Watu zaidi ya 7 wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa risisi nje ya mskikiti mmoja kusini mwa Ufaransa. Polisi wanasema kuwa hawachukulii kisa hiki kuwa cha kigaidi.


Waumini waliokuwa wakiondoka kwenye msikiti wa Arrahma, baada ya swala ya Alfajiri, walishambuliwa na washukiwa wawili waliokuwa na bunduki, nje ya msikiti huo. Watu walioendesha kisa hicho hawajulikani.

Polisi imesema imeanzisha uchunguzi ili kutambua watu hao.

Miongoni mwa waliojeruhiwa wanne ni kutoka familia moja, akiwemo msichana wa miaka 7.

Wawili kati ya watu 8 waliojeruhiwa wamelazwa hospitalini, kwa mujibu wa vyanzo vya maafisa wa usalama.

Walioshudia wanasema kuwa watu kadhaa karibu na msikiti walianza kukimbia wakati waliona washukiwa wawili wakiondoka kwenye magari yao na kuwakaribia wakiwa na bunduki mkononi.

Visa kama hivi vimekua vikiripotiwa siku za hivi karibuni nchini Ufaransa. Hivi karibuni polisi ya Ufaransa ilifaulu kumkamata mtu mmoja katika jiji la Paris baada ya kujaribu kuendesha gari kwa kasi mbele ya umati wa watu nje ya msikiti mmoja nchini humo. Kwa mujibu wa maafisa wa usalama mtu huyo alikua na lengo la kuua kwa makusudi.

Polisi inasema kwamba inaendelea kumshikilia mtu huyo, na tayari uchunguzi umeanzishwa ili kujua kwamba alishirikiana na watu wengine katika kitendo hicho.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vilisema mshambuliaji huyo ana asili ya Armenia.

Shambulizi hilo lilitokea katika kitongoji cha Créteil na hakuna aliyejeruhiwa.

Miaka miwili iliyopita Ufaransa ilikumbwa na mashambulizi ya kigaidi na kusababisha vifo vya watu wengi.

google+

linkedin