wanasayansi wasema wanaume wazee huzalisha watoto werevu | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Wednesday, 21 June 2017

wanasayansi wasema wanaume wazee huzalisha watoto werevu



Wanaume wanaochelewa kuanza familia wana uwezo wa kupata wavulana werevu kulingana na utafiti.

Watoto hao huwa werevu, wenye malengo kulingana na utafiti huo uliofanywa na chuo cha Kings College mjini London.

Umri wa mama huwa hauna athari yoyote na wasichana huwa na kinga.

Mwanasayansi mmoja anasema kuwa iwapo wanaume wataendelea kuchelewa kuanzisha familia basi tunaelekea katika jamii yenye watu werevu mno watakaoweza kusuluhisha matatizo duniani.

Matokeo ya utafiti huo ni habari njema katika sayansi .

Tafiti zilizorejelewa zimeonyesha kuwa manii ya mtu mzee hukumbwa na matatizo ya jeni na kwamba watoto huzaliwa na ugonjwa wa kiakili.

Watafiti waliwaangazia pacha 15,000 walioshiriki katika utafiti uliokuwa ukichunguza ukuwaji wao.

Kundi hilo la watafiti baadaye walichapisha tabia za watoto hao wakati wakiwa na umri wa miaka 12 .

Wale waliochunguzwa walionekana kufanya vyema shule hususana katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na uhasibu.

google+

linkedin