Waislam katika eneo zima la Mashariki ya Kati wanasherehekea siku ya kwanza ya Eid al-Fitr, sikukuu inayoashiria mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadan.
Rais wa Marekani Donald Trump ametuma salamu za Eid kwa waislam wote wanaoadhimisha sikukuu hii,akikumbusha umuhimu wa huruma na wema huku utawala wake ukivunja desturi ya kuandaa shughuli ya kutambua kumalizika kwa mwezi Mtukufu
Trump amesema kuwa pamoja na waislamu duniani kote , Marekani inakumbuka wajibu wake kuheshimu matendo ya huruma na wema
Tangu utawala wa Bill Clinton Marekani imekuwa na desturi ya kuandaa tukio kuashiria sikukuu ya Eid al Firt
Wakati huo huo Vikosi vya usalama vya ufilipino vimetangaza saa nane za kusitisha mapigano leo Jumapili, katika opelesheni yake inayoendelea dhidi ya wanamgambo wa kiislma wanaodhibiti mji wa Marawi ili kuruhusu wakaazi wa mji huo kusherehekea Eid al Fitr.