SIMBA YAPATA UDHAMINI KWA KAMPUNI YA SPORTPESA | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Sunday, 14 May 2017

SIMBA YAPATA UDHAMINI KWA KAMPUNI YA SPORTPESA

Klabu maarufu ya kandanda nchini Tanzania, Simba, imepata udhamini wa miaka mitano kutoka kwa kampuni ya SportPesa ambayo wiki hii imezindua rasmi uchezaji wa kamari kwa kubashiri matokeo ya kandanda nchini humo.
Udhamini huo wa donge nono ulitangazwa wakati wa mechi ya ligi ya Vodacom kati ya Simba aka Wekendu wa Msimbazi na Stand United ya Shinyanga katika uwanja wa kitaifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika uwanja huo, mkurugenzi wa usimamizi wa SportPesa nchini Tanzania Abbas Tarimba amesema huo ndio mwanzo tu, na kwamba timu zingine zitafaidika kwani kampuni hiyo inataka kubadilisha kabisa sura ya michezo nchini Tanzania.


``Tutafanya mpango wa mechi za kirafiki kati ya Simba na timu kubwa za nga'mbo tukitumia ushirikiano wetu na vilabu vya England kama vile Hull City, Arsenal na Southampton lengo kubwa likiwa ni kuwapa wachezaji wa Simba nafasi ya kucheza kandanda Ulaya,'' amesema Tarimba.
Wakati wa hafla hiyo, wachezaji wa Simba walivaa jezi zilizokua na nembo ya SportPesa katika kipindi cha pili huku wakishangiliwa na mashabiki wao.
Miongoni mwa walioshudia hafla hiyo ni mkurugenzi mkuu wa SportPesa nchini Tanzania, Pavel Slavkov, Tarimba na Rais wa Simba Evans Elieza Aveva na mdogo wake Geoffrey Nyange Kaburu.

google+

linkedin