Maafisa wa polisi watano wameuawa kwa bomu lililokuwa limetegwa barabarani huko Kenya mpakani na Somalia katika kijiji cha Liboi mapema Alhamisi.
Bomu lililokuwa limetegwa barabarani limewaua askari wawili wa Kenya karibu na mpaka wa Somalia katika kijiji cha Liboi mapema Alhamisi.
Hiyo ni siku moja baada ya mabomu mengine mawili kulipuka na kuua maafisa tisa, afisa usalama amesema.
"Maafisa hao watano waliuawa na bomu hilo wakati wakiwa njiani kuelekea eneo la Liboi kuongeza nguvu za operesheni za kijeshi majira ya saa nne asubuhi," amesema Mratibu wa Eneo la Kaskazini-Mashariki akiashiria kuwa ni mji ulioko mpakani na Somalia.
Kwa mujibu wa polisi, vifo hivyo vimefanya idadi ya maafisa wa usalama wa Kenya waliouwawa na mabomu ya barabarani kufikia 14 katika kipindi cha siku mbili zilizopita.
Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba huu ni mfululizo wa mabomu ambayo wanamgambo wenye itikadi kali wa Somalia wamedai kuhusika na kuyapandikiza katika maeneo mbalimbali.
Vyanzo vya habari vinasema hilo linaonyesha ugumu ambao serikali ya Kenya inakabiliana nao wakati ikijaribu kudumisha usalama nchini kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Agosti 8.