SABABU 3 ZINAZOFANYA MAREKANI ISHINDWE KUIVAMIA N.KOREA KIJESHI | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Friday 4 August 2017

SABABU 3 ZINAZOFANYA MAREKANI ISHINDWE KUIVAMIA N.KOREA KIJESHI




Licha ya kua marekani imeiwekea vikwazo nchi ya korea ya kaskazini lakini bado nchi ya korea imekua ikizidi kufanya majaribio ya makombola ya masafa ya kati yanayojulikana kama MRBM (medium range ballistic missile) na masafa marefu ambayo yana uwezo wa kuruka bara moja na jingine haya hujulikana kam ICBM (inter-continental ballistic missile) , Ambapo jaribio la makombola ya masafa marefu yalifanikiwa wiki iliyopita huku wataalamu wa kijeshi wakisema kwa sasa nchi ya korea makombola yake yana uwezo wa kufika sehemu yeyote ya marekani.

SIFA YA MAKOMBOLA

Ili kombola lipate sifa lazima liwe na uwezo wa kufika baadhi ya kilometa ni kama ifuatavyo;

Mfano kombola ili liitwe la masafa ya kati lazima liwe na uwezo wa kufika umbali kuanzia kilometa 1000 hadi 3500 ndio huitwa la masafa ya kati AU MRBM
Na nchi ya korea ya kaskazini wana makombola aya ya aina nyingi yakiwa na uwezo tofauti kama ifuatavyo

1.Rodong-1 ,lina uwezo  wa kufika kilometa kuanzia 1000 hadi 1500 ambalo lilianza kutumika mwaka 1998 lina urefu wa mita 15.6 na upana wa 1.25.
Hii ndiyo Nodong-1

2.Hwasong-10 au huitwa RD-B Musudan lina uwezo wa kufika kilometa 2500 hadi  4000  lilianza kutumika mwaka 2016 lina urefu wa mita 12 na upana wa mita 1.5
HII NDIYO HASWONG-10

3.KN-11 ina uwezo wa kufika  kilometa 500 hadi 2000 na inatumika kutoka kwenye manowari au submarine imeanza kutumika 2016 pia zipo aina hii za makombola kama KN-08 & 15 Pia hujuikana kama PUKKUKSONG -1pia jingine ni Pukguksong-2 yote yakiwa na kazi moja (2500 hadi km 3000)


Hili kombola jaribio lake lilifanyika mwezi wanne baada ya kuazimishwa kwa kuundwa taifa la korea na lilirushwa kutoka kwenye manowari ya jeshi la korea ya kaskazini

SIFA YA KOMBOLA LA MASAFA MAREFU (ICBM)
Lazima liwe na uwezo wa kufika umbali wa kilometa kuanzia kilometa 5500 na kuendeelea.
Mfano wa makombola ya masafa marefu kutoka korea ni kama ifuatavyo,

KN-08 Au huitwa Hwasong-13 linaishia kilometa 12000


Hili ndilo KN-08


Jingine ni HWASONG-14 Limeanza kutumika 2017 urefu ni 19.5 mita na upana ni 1.70 mita ,lina uwezo wa kufika kilometa hadi 10000
Hii ndiyo Hwasong-14 iliofanyiwa majaribio siku kadhaa ziizopita


SASA  ZIFUATAZO NI SABABU KWA NINI MAREKANI ANAOGOPA KUIVAMIA KOREA YA KASKAZINI KIJESHI

1.KUWEPO KWA MIZINGA MIKUBWA(artillery)
Hii mizinga ina uwezo wa kufika korea ya kusini kwa umbali wa kilometa 40 na mji mkuu wa korea ya kusini upo na mile 35 kutoka  mpakani ,na kufanya nchii ya kusini kua karibu na uhanga wa vifaa hivi kutoka kaskazini

.


2.JESHI LA ARDHINI (ground forces)

Korea ya kaskazini ina wanajeshi wa akiba wapatao 7.7 milioni huku walioko kazini ni 1.2 hivyo na kufanya korea kua na jeshi kubwa Pia wana vikosi maalumu na makomando wapatao 200000 wao wakiwa na lengo la kuivamia korea ya kusini kupitia ndege ya kirusi aina ya Antonov An-2 biplane,kupitia njia za ardhini n.k ,Hizi njia zote zitatumika wakati wa vita tuu.hapa ndipo marekani anapoogopa kwani hawa makomando wanakazi ya kuharibu maghala yao na kutekeleza mauaji ya viongozi wa kusini.
hiki ndio kikosi cha makomando wa korea ya kaskazini


TAZAMA VIDEO YAO


3.Kuwepo kwa nyuklia 
nazan kila mtu anajua uwezo wa silaha hizi endapo marekani akaanzisha vita kwa sasa itakua hatari kwa nchi yake na washirika wake kama japan ,korea ya kusini n.k

SINA LA ZIADA NIKUTAKIE USOMAJI MWEMA NA USISAHAU KUSHARE KWA MARAFIKI KAMA UMEIPENDA HII MAKALA

IMELETWA NA 
VASILY RICHARD.

google+

linkedin