Waziri wa usalama wa Kenya afariki ghafla | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Friday 7 July 2017

Waziri wa usalama wa Kenya afariki ghafla



Waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya, Meja mstaafu Joseph Nkaissery, aliaga dunia Jumamosi asubuhi katika hospitali ya Karen, kilomita chache kutoka mjini Nairobi.


Afisa mmoja katika ikulu ya Nairobi ambaye hakutaka jina kale litajwe kwa sababu hana idhini ya kuzungumza na vyombo vya habari aliiambia Sauti ya Amerika kwa njia simu kwamba Nkaissery alikuwa ameenda hospitalini ili kukaguliwa na madaktari na wauguzi.

Hata hivyo, hakutoa habari zaidi juu ya kile kilichosababisha kifo chake.

Baadaye, afisa mwandamizi katika ikulu, Joseph Kinyua, alitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari kuthibitisha kifo cha waziri huyo.

Kabla ya kulalamika kwamba hakuwa anajihisi vizuri, Nkaissery alikuwa ameandamana na rais Uhuru Kenyatta wakati wa mkutano wa maombi ya kitaifa uliofanyika kwenye bustani za Uhuru Park Ijumaa.

"Alionekana mwenye afya lakini baadaye akasema alihitaji kwenda hospitalini kwa ukaguzi," mtu mmoja ambaye hakutambulishwa, amenukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema.

Aliteuliwa kama waziri wa uslama wa ndani mnamo tarehe 2 Desemba 2014, kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Joseph Ole Lenku.

Kabla ya uteuzi huo, alikuwa mbunge wa chama cha upinzani, ODM, akiwakilisha eneo bunge la Kajiado ya Kati.

Amefariki akiwa na umri wa miaka 68.

Vyanzo vya habari viliarifu kwamba mwili wa marehemu ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha Lee Funeral Home, ambako jamaa na marafiki walionekana kuwasili wakiwa na majonzi asubuhi ya Jumamosi.

google+

linkedin