Trump kufufua vikwazo dhidi ya Cuba | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Thursday 15 June 2017

Trump kufufua vikwazo dhidi ya Cuba

Image result for trump sanction in cuba

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutangaza mabadiliko ya sera kuihusu Cuba na kukaza zaidi kamba ya vikwazo vya usafiri ambavyo vilikuwa vimelegezwa na rais Obama.

Bwana Trump pia anatarajiwa kupiga biashara kati ya Marekani na sekta za kibiashara na kitalii katika jeshi la Cuba.

Donald Trump bado anaonekana kuwa na azma ya kubatili sera zote za mtangulizi wake Barack Obama.

Katika ziara yake mjini Miami hivi leo, bwana Trump anatarajiwa kukaza zaidi kamba katika vikwazo vya usafiri vilivyotolewa na Marekani dhidi ya Cuba.

Rais Obama alikuwa amelegeza vikwazo hivyo katika hatua ya kuimarisha uhusiano kati ya Washington na Havana.


Hata hivyo wamarekani bado wataruhusiwa kuzuru kisiwa hicho cha kikomunisti lakini kupitia makundi yaliyotambuliwa.

Biashara kati ya marekani na jeshi la Cuba katika sekta ya utalii na kiviwanda pia itatiwa kikomo na bwana Trump.

Makundi kadhaa ya kutetea haki yameitaka marekani kuendelea kuzungumza na Cuba yakisema kuwa miongo kadhaa ya kuitenga Cuba haijaimarisha haki za kibinadamu nchini humo.

google+

linkedin