Watu 400 wavamia mgodi wa North Mara Tarime | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Sunday 18 June 2017

Watu 400 wavamia mgodi wa North Mara Tarime

 
Kundi la wananchi zaidi ya 400 kutoka baadhi ya kata zinazopakana na mgodi wa dhahabu wa North Mara wilayani Tarime wanaotakiwa kuhama kupisha shughuli za uchimbaji, wamevamia mgodi huo leo (Jumapili) wakidai malipo ya fidia.


Wananchi hao ambao maeneo yao yalifanyiwa tathmini tangu mwaka 2014 bila kulipwa hadi sasa, wanadaiwa kuchukizwa na kitendo cha majina yao kukosekana kwenye orodha iliyotoka hivi karibuni.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, Andrew Sata amethibitisha kutokea kwa jaribio la kuvamia mgodi uliodhibitiwa na polisi kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.


Hakuna aliyejeruhiwa wala kushikiliwa kwa tukio hilo.

google+

linkedin