Wanajeshi wachoma moto kituo cha polisi Nigeria | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Wednesday 31 May 2017

Wanajeshi wachoma moto kituo cha polisi Nigeria


Ripoti kutoka nchini Nigeria zinasema Maafisa wa jeshi la Wanamaji wamevamia na kuchoma moto kituo cha polisi mjini Calabar kusini mwa nchi hiyo.
Maafisa wa polisi watatu wanaripotiwa kuuawa, ingawa bado haijafahamia vifo hivyo vimetokeaje.
Tukio hilo limetokea kufuatia mabishano yaliyotokea katika wanajeshi hao wa majini na maafisa wa polisi.
Ripoti zaidi zinasema maafisa hao wa jeshi la maji walirudi tena katika eneo hilo wakiwa wamejiimarisha zaidi na kuanza kushambulia kituo cha polisi, na baadaye kukichoma moto.

google+

linkedin