DAWA ZA WANAJIHAD ZANASWA UHOLANZI | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Thursday 11 May 2017

DAWA ZA WANAJIHAD ZANASWA UHOLANZI

Image result for DAWA ZA WANAJIHAD ZANASWA UHOLANZI
Amsterdam,uholanzi-Maafisa wa polisi wa Uholanzi wanawatafuta washukiwa wawili baada ya maabara ya dawa kupatikana na furushi moja la dawa zinazopendwa sana na wanajihadi.
Maafisa hao walikuwa wamebaini walikuwa wamegundua dawa bandia za Capton na kusema hawajui iwapo zilikuwa zikipelekwa mashariki ya kati.
Wakati huohuo maafisa wa maswala ya fedha walifichua wiki hii wamefanikiwa kunasa dawa milioni 37.5 aina ya Tramadol ambazo hutumiwa na wapiganaji wa IS.




Mzigo huo ulikuwa unaelekea Libya.
Maafisa wa polisi wa Itali wanasema kuwa mzigo huo ulikuwa umetoka India na ungetumika kwa sababu mbili: Kusaidia kufadhili ugaidi na matumizi kwa wanajihad ili kujisisimua na kukabiliana na shinikizo la kiakili.
Utumizi wa Tramadol ulielezewa na ripoti kuwa wa kiwango cha juu miongoni mwa wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria na huenda ilitumika katika kusababisha mauaji katika pande zote mbili za mzozo.

google+

linkedin