BOKO HARAM YATOA VIDEO IKIWAONYESHA WASICHANA WALIOGOMA KURUDI MAKWAO | maendeleo media
BREAKING NEWS
Loading...

Saturday 13 May 2017

BOKO HARAM YATOA VIDEO IKIWAONYESHA WASICHANA WALIOGOMA KURUDI MAKWAO




Kundi la wapiganaji la Boko Haram la nchini Nigeria limesambaza video inayowaonesha wasichana wa shule waliogoma kuokolewa katika sehemu ya makubaliano ya serikali ya Nigeria na kundi hilo.


Katika video hiyo ya dakika tatu mwanamke anayejiita Maida Yakubu,anayedaiwa kuwa ni mmoja kati ya wasichana waliotekwa na kundi hilo mnamo April 2014,anaonekana akiwa amevalia hijabu nyeusi na amebeba bunduki.


Akiwa amezungukwa na wanawake wengine watatu waliovalia mavazi kama yake Maida alikiri kutii kundi la Boko Haram, lililogharimu maisha ya zaidi ya watu elfu ishirini tangu lililpoanzisha vurugu dhidi ya serikali ya Nigeria mwaka 2009.

Akijibu swali la mwanaume anayesikika akimuuliza kwa nini hataki kurejea kwa wazazi wake mwanamke huyo alidai kuwa ni kwasababu wazazi wake wanaishi katika mji wa wasio na imani,na kuwataka kuukubali Uislamu.

Juma lililopita takribani wasicha 82 waliotekwa miaka mitatu iliyopita huko Chibok waliachiliwa huru baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali ya Nigeria na kundi hilo.

Msemaji wa Ikulu Garba Shehu alibainisha kuwa msichana mmoja pekee alikataa kurejea kwa wazazi wake kwa kuwa aliolewa na mmoja wa wapiganaji wa Boko haram.

google+

linkedin